KITETO WASUMBULIWA NA UGONJWA WA MIMEA YA MAHINDI

Wakulima wilayani Kiteto mkoani Manyara, wanakabiliwa na tatizo linaloathiri mimea ya mahindi.

Hali hii imetishia ustawi wa maendeleo yao na kuitaka Serikili kupitia maafisa Kilimo kuingilia kati.

Toka ugonjwa huo upate kuibuka katika maeneo ya pori namba moja, mbili, kisima, na njaniodo wilayani humo, wakulima hao wamedai kutofikiwa na wataalam

Wamesema pamoja na kutoa taarifa juu ya tatizo hili wameambulia kupewa maneno ya Faraja huku wakiendelea kuathirika na tatizo hilo

Taarifa za uhakika kutoka idara ya Kilimo Kiteto zinaeleza kuwa taarifa hiyo imewafikia na kwamba jitihada zinaendekea kutaka kutatua tatizo hilo

Robert Urasa ni Afisa Kilimo Kiteto ameahidi kudhibiti tatizo hilo kabla halijakua

Maoni