Bi.Biubwa Ibrahimu, ni mkurugenzi wa kampuni ya Namaingo amekuwa wa kuigwa kwa kuimarisha watu kiuchumi.
Akiwa na kampuni yake ya Namaingo, amewezesha vikundi mbalimbali kiuchumi kwa kuwapa elimu pamoja na mbinu mbalimbali za kujinasua na Umaskini
Hatua hii imeelezewa kuwa njema hasa katika kipindi hiki kuunga mkono jitihada za Rais Dr. John Pombw Magufuli ya hapa kazi tu
Vikundi hivyo vimekuwa vikijishughulisha katika nyanja mbalimbali za Kilimo cha kibiashara
Wanalima matunda mipapai, mbogamboga,nyanya, ufugaji wa kuku, ng'ombe, na hata sungura
Ikiwa ni njia bora ya kuwafanya Watanzania kufanya kazi, tena zenye tija katika kipindi hiki ambacho Serikali imewataka wananchi kufanya kazi
Kwa sasa anasisitiza kupitia muamvuli wa namaingo kuwa umaskini hauna nafasi.
Maoni
Chapisha Maoni