*MAELEZO YA MKUU WA MKOA WA MANYARA MHE. ALEXANDAR MNYETI KUHUSU KUKAMILIKA KWA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA UKUTA KUZUNGUKA MIGODI YA TANZANITE MERERANI, MKOANI MANYARA .*
Maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite hapa Mirerani yamekamilika kwa asilimia mia moja.
Niwasihi wananchi wa Mkoa ya Manyara na Mikoa ya Jirani kujitokeza kwa wingi kesho tarehe 6 Aprili 2018 katika uzinduzi wa ukuta utakaofanyika hapa Mirerani.
Ujenzi wa ukuta huu unatokana na Dhamira ya dhati ya Rais Wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Jukumu la Kulinda ukuta huu ni la wananchi wote kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.
Watanzania wote wamefurahia ujenzi wa ukuta huu Kwa kuwa unalenga kulinda rasilimali zetu.
Wananchi wote wa Mkoa wa Manyara wanaunga juhudi za Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli katika Kulinda rasilimali za Taifa yakiwemo madini.
Ushirikiano kati ya Jeshi letu la Wananchi Tanzania (JWTZ) na wananchi ni mzuri kwa kipindi chote cha ujenzi wa ukuta hadi sasa.
Ukuta huu una urefu wa kilometa 24.5 na unazunguka eneo lote la migodi ya Tanzanite.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI HALMASHAURI YA MJI WA BABATI
Maoni
Chapisha Maoni