SAME YATAKA UWEKEZAJI VIWANDA VYA GYPSUM.

SAME YATAKA UWEKEZAJI VIWANDA VYA GYPSUM.

💠Ukaguzi wa barabara na maeneo ya uchimbaji madini ya Gypsum Eneo la Chankoko, kata ya Makanya, Same.
💠Ni ziara ya Kamati ya ulinzi Same, Ofisi ya madini Mkoa na wataalamu wa Halmashauri.
💠Wakutana na wachimbaji na wasafirishaji wa madini hayo
💠 Barabara ni changamoto kubwa.
💠Waonyesha uzalendo, wakubaliana kuchangia kuziba makorongo wakati tunasubiri maombi serikalini. Serikali yaahidi kushughulikia haraka.
💠Wako tayari kulipa kodi zote za kisheria. Waomba kikao na DED.
💠Wakumbushwa kusawazisha udogo baada ya kuchimba na kupanda miti,  pia kuwepo vyoo. eneo la machimbo.
💠DC asisitiza kuanzisha viwanda vidogo vya Gypsum na  kuchakata hatua ya kwanza
💠Zaidi ya leseni 100 zafanya kazi. Eneo latoa ajira nyingi kwa vijana kwani uchimbaji watumia mikono. Ni wachimbaji wadogo. Zaidi ya vitalu 400 havijaendelezwa.
💠Wilaya yatenga hekari 4000 za uwekezaji Makanya. Wakaribisha uwekezaji wa viwanda.
💠" Pamoja na kutafuta wawekezaji wa nje, kipaumbele chetu ni Watanzania wenyewe njooni muwekeze." Alisema DC.
💠Awapongeza wanawake wanaochimba gypsum.

Maoni