TUTAPANDA HADI KILELE CHA MLIMA SHENGENA

⛰TUTAPANDA HADI KILELE CHA MLIMA SHENGENA ⛰

🇹🇿Tukiwa kileleni tutapaza sauti kuwaeleza watanzania mlima mrefu upande wa Tao la mashariki baada ya mlima Kilimanjaro.

🇹🇿Ndipo mahali ambapo mlima Kilimanjaro unaonekana vizuri kuliko mahali pengine popote.

🇹🇿" Kuanzia mwezi Mei, 2018 tutafanya mazoezi ya mfululizo ili tujiandae kufika kileleni. hatutaki kuishia katikati, kila mtu ajiandae na tuvae tshirts zetu za Same tukajitangaze; Hakuna wa kuisemea Same juu ya utalii huu zaidi yetu sisi" Maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Same, Mh. Rosemary Senyamule.

🇹🇿 Najua iko shida ya barabara, Lakini nawahakikishia serikali ya awamu ya tano ya Mh. Dr. John Pombe Magufuli imekwisha leta hela za kuanzia matengenezo Tshs. 700M. na Itaendelea kuleta kadiri uwezo unavyoongezeka.

🇹🇿 Tunataka kukuza utalii huko na nchi ifaidike, asiyeweza kufika kilele cha Kilimanjaro, aje apande Shengena atafika kileleni.

🇹🇿Hayo yalisemwa wakati wa siku ya mazoezi ya kila jmosi ya pili ya mwezi Tar. 15/04/2018 yaliyofanyika uwanja wa kwasakwasa.

🇹🇿Mwalimu machachari aliyetoa mazoezi hayo bila kujali kuwa kuna wahenga; alipelekea kila mara wahenga kudai mazoezi yabadilishwe.

🇹🇿Raha ya mazoezi hiyo, wazee na vijana pamoja.👯🏼‍♀👯🏽‍♂🏃🏽‍♀🏃🏽‍♂

" Same is not same"

Maoni