KIBAYA MSISUKUMWE KUFANYA USAFI
Imekuwa ni mazoea sasa ili mji wa Kibaya Kiteto uwe safi, viongozi wanalazimika kuwatangazia wananchi kufanya usafi kila kaya.
Kimsingi hili halina Afya katika maendeleo ya eneo husika na hata Afya za watu kwa ujumla.
Jukumu la kufanya usafi ni la mtu mwenyewe, yeye ajipime pale alipo kama yuko sahihi kusukumwa kufanya usafi.
Haiwezekani mtu mwelewa eti mpaka akamatwe na migambo na kulazimishwa kufanya usafi.
Hayo yote mwisho wa siku kinachosisitizwa ni Afya ya mtu binafsi ili aweze kuishi tena bila kuugua.
Uchafu una madhara mengi yakiwemo kusababisha kupata magonjwa na kuhatarisha maisha ya mtu.
Napia utalazimika kutumia Pesa kujitibu wakati ungeweza kuzitumia kwa shughuli zingine za maendeleo.
Na ule muda wa kujitibu ungeweza kufanya shughuli zingine za maendeleo hivyo ni jukumu la mtu mwenyewe kujipima.
TAFAKARI HILI..KAMA KUNA ULAZIMAWA KUSIMAMIWA KUFANYA USAFI?
Maoni
Chapisha Maoni