UZALENDO NI KUAMUA KUFANYA KWA AJILI YA NCHI YAKO

UZALENDO NI KUAMUA KUFANYA KWA AJILI YA NCHI YAKO.

💎 Ni wachimbaji na wasafirishaji wa madini ya Gypsum eneo la Chankoko kata ya Makanya - Same.

Wameamua kumwaga molam kwenye barabara ili kuziba mashimo kwa barabara wakingoja mpango wa serikali juu ya barabara hiyo.

💎 Wasema watatoa muda wao na nguvu zao kufanya barabara ipitike kwa sasa
💎DC wa Same aanzisha shime hiyo kwa kutoa mafuta lt. 100.

Pia awaahidi gari la kubebea molam toka halmashauri.

💎Aahidi kufuatilia mpango wa ujenzi toka TARURA kwani barabara iko kwenye mpango.

💎Kazi yaanza mara moja ili kunusuru soko la gypsum ya Same.

DC atoa wito kwa wananchi wote. Shime hii ifanyike kila mahali kwani mambo ya kufanya kwenye maendeleo bado ni mengi.

Awapongeza mno wananchi hao wa Chankoko.

Maoni