Wabunge Manyara wakabidhi mabati 230

Viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini  Mhe. Jitu Soni wametoa mabati 230 kusaidia jitihada za wananchi wa Kata ya Gallapo ktk ujenzi wa jengo la Upasuaji kituo cha Afya Gallapo.

Katika jitihada hizo wabunge wa Mkoa wa Manyara wakiongozwa na Mbunge wa Hanang Mhe. Dkt Mary Nagu wamechangia Tsh1,400,000.

Wakitoa salamu kwa wananchi wa Kata ya Gallapo Wabunge hao wakisisitiza kufanya kazi kwa bidii na kuchangia shughuli za maendeleo

Hatua ya ujenzi huo imefikia sehemu ya kupaua hivyo bati hizo zitasaidia katika kukamilisha huduma hiyo ya afya

Mwisho.

Maoni