Wanafunzi 84,354 kunywa dawa za minyoo Babati

Watumishi wa Idara Afya na Elimu wa halmashauri ya Babati wametakiwa kusimamia vyema na kwa weledi  zoezi la umezeshaGBji Dawa za MinyooTumbo katika shule za Msingi.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Babati, Hamisi Idd Malinga, katika kikao cha utekelezaji wa zoezi hilo akiwa na maofisa elimu, afya na waratibu amewataka kuwa makini

"Tumieni Elimu, uzoefu na weledi kuhakikisha zoezi la umezeshaji dawa za minyootumbo kwa wanafunzi wa Shule za msingi linafanikiwa Kwa kiwango kikubwa"

Amesema kufanikiwa zoezi hilo kutafanya watoto wakue vizuri na kukuza uwezo wa ufahamu na uelewa Shuleni.

Mratibu wa zoezi hilo James Mleli amesema zoezi hilo  litaanza na uhamsishaji ngazi ya vitongoji, vijiji na shule ili kuwapa Jamii uelewa na umuhimu wa kumeza dawa hizo.

Umezeshaji dawa za minyoo tumbo kwa halmashauri ya Babati  linategemewa Kufanyika tarehe 19/4/2018 kwa shule za msingi 143 zenye wanafunzi 84,354 na kuanzia umri wa mpaka 5 hadi 17 wanategemea kumeza dawa hizo.

Maoni