WANAUME WA SAME NA KAULI YA HAPA KAZI TU

HAPA KAZI TU

Ni Maneno yaliyosemwa Na wanaume wa Kijiji cha ngarito, kata ya Gavao saweni, Wilayani Same. Baada ya kumaliza kazi ya kusafisha Barabara urefu wa km. 4 kwa msaragambo.

Waomba kupata umeme, walimu na Barabara, na kujibiwa kuwa mipango ya umeme, watapata mwaka ujao.

🔸 TARURA watakiwa kuingiza Barabara hiyo kwenye mfumo ili itambulike.
🔸Wahimizwa kuendeleza msaragambo kila Jumatatu ili kupata maendeleo kwa haraka.

🔸"Barabara nyingi ziliitwa za vijiji Na hazikuwepo kwenye mfumo wa serikali, hii ilipelekea Wilaya ya Same kupata bajeti ndogo ya fedha za Barabara".

DC Same amewasisitiza TARURA Kuhakikisha wanapitia Barabara zote Na kuziingiza kwenye mfumo ili urefu wa Barabara zinazohudumiwa Na serikali ziweze kuakisi ukubwa wa Wilaya ya Same. Hii itapelekea kuongezewa bajeti ya Barabara.

🔸Awapongeza kwa kung'oa mirungi yote Na kuwasisitiza kupanda kahawa.
"Nitafikisha taarifa hizi ngazi za Juu, kuwa wananchi wa Ngarito wamesikia wito wa serikali wa kuacha Madawa ya kulevya" Alisema DC Same.

🔸Aagiza idara ya Kilimo kuhakikisha wanawapa maelekezo Juu ya mazao mengine mbadala.

Maoni