Watoto 2200 walemavu huzaliwa kila mwaka

PATRICIA KIMELEMETA

ZAIDI ya watoto 2200 wanazaliwa na nyayo za kupinda kila mwaka na kusababisha kupata ulemavu wa kudumu kama hawajafanyiwa upasuaji mapema.

Hayo yalisemwa na Daktari bingwa wa upasuaji wa mifupa wa Hospitali ya ÇCBRT,Prosper Alute wakati wa zoezi la upasuaji wa watot wenye matatizo hayo.

Alisema kwa siku, hospitali hiyo inawafanyia upasuaji watoto zaidi ya 17 kwa kutumia vifaa maalumu ili waweze kurudisha nyayo zao kwenye hali ya kawaida.

"Kwa sasa tatizo hili linaongezeka siku hadi siku jambo ambalo linahitaji mkakati wa pamoja wa kuhakikisha watoto wenye matatizo kama hayo wanafanyiwa upasuaji," alisema Dk. Alute.

Alisema hospitali hiyo imeweza kushirikiana na watalaamu kutoka mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kutoa matibabu bure kwa watoto hao.

"Kwa siku tunaweza kuwafanyia upasuaji watoto zaidi ya 17 kwa siku wenye nyayo zilizopinda na kurudisha miguu yao kwenye hali ya kawaida ili waweze kutembea kama watoto wengine," alisema.

Naye Mtaalam mwingine wa upasuaji wa mifupa Dk. Robert Mhina alisema kuwa madhara ya mtoto mwenye nyayo hizo ni pamoja na kuwa  na maumivu makali wakati wa kutembea na kushindwa kutembea vizuri.

Alisema idadi kubwa ya watoto hao hukumbana na changamoto za kunyanyapaliwa na kutengwa na jamii na wakati mwingine kama hajatibiwa anaweza kuwa na ulemavu wa kudumu.

"Watoto wengi wanapata matatizo ya kushindwa kutembea kutokana na ulemavu wa miguu, hivyo basi wazazi wanaweza kuwafikisha kwenyw hospitali ya CCBRT ili waweze kupatiwa matibabu ni bure," alisema.

Mwisho

Maoni