WAZUNGUMZIA KIFO CHA MKURUGENZI KONGWA

KAULI ya Mkurugenzi wa wilaya ya Simanjiro, Myenzi kuhusu ajali ya mkurugenzi mwenzake wa Wilaya ya Kongwa

NDUGU ZANGU NASIKITIKA KUWAJULISHA KUWA MKURUGENZI MWENZETU WA HALMASHAURI YA KONGWA NDUGU NGUZA IZENGO AMEFARIKI DUNIA KWA AJALI YA KUANGUKIWA NA TANKER LA MAFUTA JANA USIKU.

MUDA HUU NDIO CRANE IMEONDOA TANKER LILILOKUWA LIMELALIA GARI LAKE.

TULIKUWA NAYE JAPAN OKTOBA NA NOVEMBA MWAKA JANA MWENYEZI MUNGU AMREHEMU

KAULI ZA BAADHI YA WANANCHI

Hili ni pigo kwa watanzania na Halmashauri ya kongwa Mungu awajalie familia uvumilivu katika kipindi hichi kigumu

Mery Margwe: Mwandishi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesikitishwa na taarifa ya ajali ya gari iliyompata Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ndugu Ngusa Izengo iliyotokea usiku WA kuamkia leo  katika eneo la Chalinze Nyama nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Taarifa kamili juu ya ajali hii mtajulishwa baadaye.

Inetolewa n'a Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Ofisi ya Rais TAMISEMI
16/04/2018

Maoni