*MKUU WA WILAYA YA KONGWA NDEJEMBI AAGIZA POLISI KUWATIA NDANI MGANGA MKUU WA KITUO CHA AFYA, MHANDISI WA HALIMASHAURI NA MKUU WA KITENGO CHA MANUNUZI*
Mkuu wa wilaya ya kongwa amewatia ndani watajwa juu hapo kwa kushindwa kusimamia mradi wa ujenzi wenye thamani ya million 400 wa kituo cha afya Mlali wilayani Kongwa. DC Ndejembi alisema, fedha hizo zimetolea na serekali chini ya uongozi wa Rais Dr John Pombe Magufuli, na ni kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho ili kitoe huduma kwa wananchi.
DC Ndejembi alisikitishwa na kasi ya ujenzi huo baada ya kutembelea ujenzi huo leo 7/5/18 akiwa kwenye ziara ya kutembelea kata za Mlali na Chiwe na kugundua ujenzi ulisimama kwa uzembe kwa siku 27.
Mganga mkuu anatuhumuwa kuchelewesha malipo ya mkandarasi kwa kudai rushwa ya laki 5 na kuchelewesha malipo hadi atakapo pewa fedha hizo na hivyo DC kuagiza TAKUKURU kushugulikia swala hilo.
Vile vile mhandisi anadaiwa kuchukua posho ya laki 9 na kuto fika kusimamia kazi hio kama alivyo takiwa. Idara ya manunuzi walinunua vifaa kwa gharama kubwa kulingana na uhalisia wa bei.
Maoni
Chapisha Maoni