DC Mbulu kutatua tatizo la wizi wa mifugo.



Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga, amefanya mkutano wa ujirani mwema kutatua tatizo la wizi wa mifugo.

Mkutano huo umehusisha kata za Dirim, Dinam, Yaeda chini, Eshkesh, na Endamilay, ukilenga kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya wizi wa mifugo.

Akiongea na wananchi wa kata hizo,Mkuu huyo wa Wilaya, amepiga marufuku kusafirisha mifugo bila vibali ndani na nje ya wilaya.

Pia ameagiza watendaji wa vijiji na kata kuwa na daftari la wageni na kwamba, pasiwepo mgeni atakayeingia vijijini bila taarifa kwa viongozi.

Katika kujenga mahusiano kwenye kata hizo ameagiza kuundwa kwa kamati za wazee kumi kutoka kila kijiji ili kukutana na mkuu huyo wa wilaya kuzungumzia ulinzi na usalama na ushirikiano baina ya kata zao.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza wananchi kuamini vyombo vya dola badala ya kuchukua sheria mkononi.

Mwisho.

Maoni