HALMASHAURI ZAAGIZWA KUWAPA WAUGUZI STAHILI YAO YA SARE ZA KAZI

HALMASHAURI ZAAGIZWA KUWAPA WAUGUZI STAHILI YAO YA SARE ZA KAZI

💠Ni siku wa sherehe ya wauguzi Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika Wilayani Same.

RC Kilimanjaro Mh. Anna Mghwira aliyekuwa mgeni rasmi amewaagiza wauguzi kutimiza wajibu wao ili wasiingiliwe, kwani wasipotimiza wajibu ni lazima wataingiliwa.

Aagiza halmashauri ambazo hazijawapa Sare, kufanya hivyo.

Awapongeza kwa kazi nzuri  wanayoifanya Na Kutaka watu wote tuwatie moyo kwani ni kazi ya wito.

💠Naye Mkurugenzi wa Wauguzi Tanzania toka Wizara ya Afya Ndugu Moyo aliyehudhuria sherehe hiyo kwa niaba ya Ktb. Mkuu.
Alitoa salamu za Wizara Na kutoa ufafanuzi wa maombi yaliyojitokeza kwenye risala ya wauguzi.
Awataka wauguzi kuweka maazimio wanayotaka kuyafikia kila mwaka wanapo kula kiapo.

💠Yaelezwa wauguzi wanaweza kuokoa vifo vya mama Na Mtoto kwa 70% bila msaada mwingine.

Sherehe iliadhimishwa kwa kutoa Huduma kwa jamii kwa kupima sukari, BP, HIV Na Huduma ya kutoa damu ambapo chupa 30 zilipatikana.

Siku hiki huadhimishwa Tar. 12 Mei ya kila mwaka kumkumbuka  muasisi wa wauguzi duniani Ndugu Florence Nightngare. Zawadi zilitolewa kwa wauguzi bora.

Maoni