Hanang kunufaika na uwekezaji wa SUMAJKT

Mkurugenzi mtendaji wa SUMAJKT, Brigadia Jenerali Charo Yateri, akitaja miradi itakayowanufaisha wananchi wa Wilaya ya Hanang mara baada ua kutembelea eneo la ekari nne walilopewa na halmashauri kwaajili ya uwekezaji wa ujenzi wa Hoteli ya hadhi tano (five star) na maduka ya karakana..kulia ni Bi. Sarah Msafiri Mkuu wa Wilaya ya Hanang.
Mkurugenzi mtendaji wa SUMAJKT, Brigadia Jenerali Charo Yateri, akitoa ufafanuzi wa uwekezaji katika wilaya ya Hanang kwa viongozi mbalimbali Wilayani humo
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi. Sarah Msafiri akizungumza na vyombo vya habari kwa kuwahakikishia uongozi wa SUMAJKT kuwa ataharakisha wanakamilisha taratibu za kisheria ili shughuli za uwekezaji zianze mara moja.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Hanang akifafanua namna walivyojipanga kunufaika na uwekezaji wa SUMAJKT
Makubaliano ya pamoja kati ya halmashauri ya wilaya ya Hanang na uongozi wa SUMAJKT kuhusu uwekezaji wilayani hapo..
Baadhi ya watumishi wa Serikali Wilayani Hanang wakifuatilia makubaliano ya kupeana ardhi ya uwekezaji kati ya Halm na SUMAJKT
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Sarah Masafiri akiteta na Meja Generali (msaafu) Mohamed Farah wakati wa makubaliano ya kupeana eneo la uwekezaji wilayani humo
Baadhi ya watumishi wa Serikali Wilayani Hanang wakifuatilia makubaliano ya kupeana ardhi ya uwekezaji kati ya Halm na SUMAJKT


Wananchi Hanang kunufaika na uwekezaji wa SUMAJKT

Na, MOHAMED HAMAD HANANG
WANANCHI wilayani Hanang mkoani Manyara, wanakusudiwa kunufaika na uwekezaji mkubwa utakaofanywa na shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga Taifa SUMAJKT.
Mkurugenzi mtendaji wa SUMAJKT, Brigadia Jenerali Charo Yateri, ametaja miradi itakayowanufaisha wananchi hao kuwa ni pamoja na ujenzi wa hoteli ya hadhi tano (five star).
Ujenzi wa karakana ya zana za kilimo, maduka makubwa ya bidhaa (shopping center) karakana za matrekta, kituo cha mafuta cha uhakika na uwekezaji wa  kilimo cha uzalishaji wa mbegu.
Akizungumza baada ya kuwekeana mkataba wa makabidhiano ya kupeana maeneo hayo mkurugenzi huyo alisema, lengo la uwekezaji huo ni kuunga mkono Jitihada za Serikali ya awamu ya tano za Rais Dr. John Pombe Magufuli.
Alisema SUMAJKT itaunga mkono Serikali kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda sambamba na kutengeneza nafasi za ajira kwa wananchi asemavyo Rais Dr. John Pombe Magufuli .
Alisema katika hatua za awali waataanza na ujenzi wa maduka makubwa na hoteli ya ngazi tano (five star) ambayo pia itatumiwa na viongozi wakubwa wa Kitaifa wanapofika wilayani hapo.  
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya SUMAJKT, Meja Generali (msaafu) Mohamed Farah alisema kazi hiyo itaanza baada ya kukamilishwa michoro kisha watatoa ajira kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali katika maeneo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi. Sarah Msafiri aliwahakikishia uongozi wa SUMAJKT kuwa atahakikisha kuwa wanakamilisha taratibu za kisheria haraka ili shughuli hizo zianze mara moja.
“Napata faraja kupata uwekezaji mkubwa, wananchi watanufaika kwa mambo mbalimbali kwakuwa tuna miundombinu bora ya barabara ya lami hivyo moja kati ya vitu muhimu katika uwekezaji ni kuwa na miundombinu mizuri.
“Nitoe wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli hizi kwani wao ndio wanufaika wakubwa, na ambao wanatakiwa kutoa nguvu kazi kubwa katika miradi hiyo adhimu”alisema DC Msafiri.
Kabla ya kuwekeana makubaliano ya uwekezaji huo, pande hizo zilienda kuona eneo la ekari nne zilizombwa kwaajili ya ujenzi wa hoteli kubwa na maduka ya kisasa pamoja na shamba la ekari 2000 kwaajili ya kilimo cha uzalishaji wa mbegu eneo la Bassotu ambako shughuli za kilimo zitafanyika.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Geoge Bajuta aliuomba uongozi wa SUMAJKT kuwa ajira zitakazotolewa na SUMAJKT, kipaombele kiwe kwa wananchi wa Hanang.
Alisema kwa sasa wananchi wako tayari kushirikiana na SUMAJKT kikamilifu kufanikisha miradi yote akidai kamwe hawatawaangusha katika uwekezaji huo ili uwe wenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
MWISHO.

Maoni