KUJAA MTO PANGANI KILIO KWA WAKAZI KATA YA RUVU

KUJAA MTO PANGANI KILIO KWA WAKAZI  KATA YA RUVU

💠Mto Pangani ambao umekuwa ukichangia uchumi mkubwa kwa kata ya Ruvu na  wananchi wa Wilaya ya Same. Umegeuka kero baada ya kujaa na kulazimu maji kumwagika juu ya kingo za Mto huo.

Tukio hilo limesababisha wananchi kuzingirwa na maji pia mashamba kujaa maji na kuharibu mimea.

💠Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Same  ilitembelea eneo hilo na kuona madhara hayo na kulazimika kutoa maelekezo ya uokowaji
1. Kwa kutumia teknolojia ya Drone waliweza kuona watu waliokaa juu ya kichuguu wamezungukwa na maji.
Watu hao waliokolewa na kutolewa.
2. Kuagiza wananchi wa kijiji cha Mferejini kuhama kabla maji hayajaingia kwenye nyumba na daraja halijaziba.
3. Idara ya afya kupeleka dawa na kuhakikisha tahadhari dhidi ya kipindupindu inachukuliwa.
4. Afisa elimu msingi kuweka utaratibu wa wananchi wanafunzi kuhamia shule za jirani.
5. Wataalamu kufika, kuweka mazingira ya tahadhari na kuleta taarifa haraka kama kuna mahitaji ya dharula.

💠Dalili zinaonyesha maji yanaendelea kujaa hivyo kuongeza mafuriko. Kwani baadi ya maeneo yamesambaa umbali wa km.3 kutoka mtoni.

💠Mkuu wa Wilaya ya Same Mh. Rosemary Senyamule amewaagiza Pangani kutoa taarifa kila siku juu ya hali ya mto huo.
Mpaka sasa hakuna kifo kwa mtu wala mifugo, madhara makubwa yametokea kwa mazao mashambani.

Maoni