Mwenyekiti wa MAMEC, Yusuph Dai, akimkaribisha mgeni rasmi, ambaye alikuwa mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akisema siri ya mafanikio ni
ushirikiano na mshikamano
Nico Mwaibale (mwandishi) akisoa somo kwa wadau wa habari mkoani Manyara siku ya uhuru wa vyombo vya habari mjini Bababti.
NA MOHAMED
HAMAD
Chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Manyara, ni miongoni mwa walioungana na vyama
vingine kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.
Siku hii
pamoja na mambo mengine ilikuwa na lengo la kutafakari utendaji kazi wa vyobo
hivyo kama moja ya wajibu wao katika kuwatumikia wananchi.
Wakiwa na
wadau wa habari mkoani Manyara kwa pamoja waliweza kufanya tafakuri ya namna
vyombo vya habari vilivyoweza kuchangia maendeleo ya wananchi na mkoa wa
Manyara kwa ujumla.
Mwenyekiti
wa Chama hicho, Yusuph Dai, akimkaribisha mgeni rasmi, ambaye alikuwa mkuu wa
Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alisema siri ya mafanikio ni ushirikiano na
mshikamano
“Mhe Mgeni
rasmi, nafasi ya uenyekiti niliyopata kwa kipindi hiki kifupi kuongoza hawa
wenzangu siri yake ni ushirikiano, hivyo hatuna budi kuhubiri ushirikiano na
mshikamano hasa katika kipindi hiki kwa kuwatumikia wananchi.
“Mara nyingi
huwa nasema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu..mkoa wetu wa Manyara
usingeweza kufikia hapa ulipo bila vyombo vya habari, hivyo kama chama tunaomba
tuungane pamoja ili tuweze kufikia sehemu tarajiwa”
Mkuu wa mkoa
wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza na wadau hao, alifananisha chombo cha
habari kama maji, kuwa hakikwepeki lazima kitumike hata kama hutaki.
“Ndugu zangu
waandishi wa habari wa mkoa wa manyara, nitumie fursa hii kuwashukuru sana sana..kwa
kazi zenu nzuri mnazozifanya, kama kiongozi wa Serikali natambua mchango wenu.
Huwezi
kufika popote kama hutotumia chombo vya habari..Manyara tutaendelea kuvitumia vyombo
vya habari ili tuweze kufikia malengo tarajiwa ambayo ni maendeleo”.
Katika hatua
hiyo aliwataka waandishi wa habari kuwa na subra katika kazi zao na kuacha
tabia za kulazimisha jambo hata kama wanahaki ya kupata habari wasidai na
kuwakera wengine
Akiwasilisha
mada mbili kwa pamoja ikiwemo usalama wa
wanahabari, Nico Mwaibale (mwandishi) alisema adui wa mwanahabari ni wanahabari
wenyewe.
Amewata
waandishi wa habari kufanya kazi kwa kufuata misingi na taratibu za sheria za
nchi lengo likiwa ni kuihudumia jamii kama sheria isemavyo na kuacha kufanya
kazi kwa mihemko.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni