RAHA YA KUENDA KIJIJINI NI KUTATUA KERO
Zamu hii ilikuwa ni kata ya Suji, ambapo kijiji cha Gonjanza kimepata mtendaji baada ya kukaa zaidi ya miaka 7 bila mtendaji.
🔶Wang'oa mirungi wapanda kahawa, vitalu 11 vimeanzishwa vyenye miche 36000 ya kahawa, itapandwa wakati wa mvua za vuli ambapo heka 72 zitapandwa kahawa. TACRI wametoa mbegu, Floresta - viriba na serikali utalaam.
🔶 Wafanya msaragambo kwa kusawazisha eneo la kujenga zahanati Marindi na DC Same. Wameagizwa kuanza haraka ujenzi na kukamilisha boma ili serikali imalizie. DC Achangia mifuko 20 ya cement.
🔶 Suji imekuwa ni kata ya kwanza kujengwa barabara la lami kwa kata za milimani.
🔶Waomba kuongezewa walimu, daktari(Gonjanza), maji, umeme na mpaka wa kijiji.
🔶Mkuu wa Wilaya ya Same alisema " Tunatakiwa kumpongeza Rais wetu Mh. John Pombe Magufuli kwani ametangaza kuajiri watumishi zaidi ya 52,000. Uamuzi huu unamaanisha idadi hiyo ya watu itaanza kulipwa mshahara tangu mwezi wa kuajiriwa hadi watakapo staafu.
Huu ni uamuzi mkubwa na wa kijasiri. Ni imani kuwa hata Same tutapata walimu wapya na watumishi wa afya" .
🔶Pia DC huyo akiwa na wataalamu walijibu kero zote za wananchi na kuwataka kujiunga na iCHF mwisho mwezi Julai, 2018.
Maoni
Chapisha Maoni