Ukaguzi ujenzi wa kituo cha Afya Shengena.

Ni ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha Afya Shengena.

DC Same Mh Rosemary Senyamule amekagua kituo hicho na kuagiza yafuatayo:

🔶Speed ya ujenzi iongezeke, Sababu za mazingira zisiwe kisingizio, saana zitutofautishe na wengine ambao hawakupata changamoto. Amtaka Mkandarasi kufanyakazi usiku na mchana.

🔶Ataka vifaa vyote viwepo site "Nisisikie kazi imesimama hata siku moja kwa kusubiri vifaa, mara mchanga, tofari nk., nitamuondoa huyo mzembe atakayesababisha kazi kusimama". Aliyasema Mkuu huyo wa Wilaya.

🔶Aagiza Wananchi kushiriki kusogeza vifaa ili kazi iende haraka na kuokoa hela nyingine ili zitumike kujenga korido.

Serikali imetoa Tshs. 400M kwa ajili ya kujenga wadi la wazazi, chumba cha upasuaji na jengo la maabara.

🔶Ataka taarifa ya kazi kila siku kutoka kwa mtendaji wa kata, aagiza viongozi kuanzia ngazi ya kitongoji wafike ofisini kwake ijumaa Tar. 18/05/2018.

🔶Atoa onyo kwa watumishi wanaoacha wagonjwa na  kwenda kunywa chai  wakati wa saa za  kazi.

🔶Apongeza Rais Mh. Dr. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za vituo viwili vya afya Wilayani Same."

Tulizoea kupokea fedha nusu nusu yaani kwa awamu. Lakini sasa tumeletewa fedha yote ya kumaliza ujenzi.

Hatuwezi kushindwa kusimamia, ili lengo la serikali ya CCM litimie.

" HAPA KAZI TU"

Maoni