Ni kikao cha Viongozi wa kata ya Chome kilichojumuisha Viongozi 30 kuanzia vitongoji vyote, vijiji Na kata pamoja Na DC Same.
Waagizwa kumaliza mirungi yote iliyobaki, kumaliza tatizo la ulevi na vijana watukutu.
Waahidi kuongeza nguvu kituo cha Afya Na kumaliza ujenzi kwa wakati, kwa kupeleka wananchi kufanya msaragambo.
Waagizwa kila Kijiji kuainisha eneo la kujenga soko. DC kupeleka wataalamu kuona eneo linalofaa kujenga soko la kata.
Kusimamia utunzaji wa mazingira hasa msitu wa Chome/ Shengena. Waagizwa kushika chain sew zote vijijini.
Waelezwa mipango mikubwa ya Wilaya kuifanya Chome kuwa kata ya Utalii Na umuhimu wa kuweka mipango inayoendana Na adhma hiyo.
Mh. Dr. John Pombe Magufuli ametoa Tsh. 700M za ujenzi wa barabara Na mkandarasi ataanza kazi mwezi June , 2018 mapema.
DC Aahidi kuwachukulia hatua Viongozi wote wasiowajibika, nataka maagizo haya yafanyiwe kazi Na kata Na vijiji vyote, awataka Maafisa Tarafa kuwasimamia.
" Mliwalea wadokozi wakawa vibaka; vibaka wakawa wezi na sasa wezi wanaanza kuwa majambazi.
Nataka mkatimize wajibu wenu wa kuchukua hatua Na tatizo la vijana kuanza kupiga Viongozi nisilisike teeena! "
Uongozi ni kuonyesha njia, kata ya Chome haistahili kuwa hivyo ilivyo, kwani mlisomesha watoto wengi, washirikisheni kwenye shughuli za maendeleo"
Alisema DC Same - Mh. Rosemary Senyamule.
Alisema DC Same - Mh. Rosemary Senyamule.
" Same is not same"
Maoni
Chapisha Maoni