WAADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI NGAZI YA KATA.
Ni jambo lililoleta mvuto Na kuonyesha ubunifu wa pekee, kata ya Makanya kwa kusherekea siku ya wafanyakazi kwa muundo wa kipekee.
🔸Wakutana watumishi woote ngazi ya kata.
Waeleza changamoto zao katika kata.
🔸Mgeni Rasmi ambaye pia alishiriki maandalizi hayo alikuwa ni Afisa Tarafa hiyo (Chome Suji) Ndugu Sixbert Sarmett. Ambaye alipokea kero na alihimiza ushirikiano kwa watumishi na jinsi ushirikiano unavyoweza kuboresha matokeo kwa kila idara kwani idara zinategemeana.
🔸Walifanya michezo ya kuvuta kamba/ kufukuza Kuku kama sehemu ya sherehe hiyo.
🔸Mkuu wa Wilaya ya Same, Mh. Rosemary Senyamule apongeza ubunifu huo.
Kwani unakuwa Na uwakilishi mkubwa na ngazi ya mwisho kwa wafanyakazi, unatoa nafasi ya Karibu ya kusikiliza kero Na kuongeza mshikamano kwa watumishi.
🔶Alisema " Mmetukumbusha jambo jema, hivyo ninaagiza mwaka ujao kila kata kuadhimisha siku ya wafanyakazi ngazi ya kata Na baada ya Hapo tutakusanya kero zilizotajwa kila kata Na kupata kero za Wilaya kwa uwakilishi mkubwa. Na hivyo kuzishughulikia kwa ukaribu zaidi".
Japo hii haibadili maadhimisho yanayofanywa Na ngazi ya Wilaya kwa eneo husika.
🔸Zawadi zilitolewa kwa kila idara.
" Same is not same"
Makanya is not same.
Maoni
Chapisha Maoni