Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama, akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Manyara alipowasili kuweka jiwe la msingi kituo cha afya Mirerani.
Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama, akiweka jiwe la msingi kiruo cha Afya Mirerani Simanjiro Manyara.
Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama,akikagua jengo la Kituo cha Afya Mirerani Simanjiro Manyara
Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama,akiwa na Mhandisi Zephania Chaula katika ukaguzi wa jengo la kituo cha Afya Mirerani Simanjiro Manyara.
Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama,akimjulia hali mmoja wa akinamama ambaye jina lake halikufahamika mapema aliyejifungua muda mfupi baada ya kuwasili kituo cha Afya Mirerani kuweka jiwe la msingi
Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama,akisomewa taarifa na mkurugenzi mtendaji wa halm ya wilaya ya Simajiro alipowasili kuweka jiwe la msingi kituo cha Afya Mirerani Manyara.
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAID, Dr. Leonard Maboko akitoa taarifa namna walivyopata wazo la kusaidia ujenzi wa Kituo cha Afya Mirerani Simanjiro Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula, ambaye pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti katika zoezi la kuwekwa jiwe la msingi kituo cha Afya Mirerani na Waziri Jenista Mhagama.
Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama, akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Mirerani alisema wanaume wasitumie wake zao kujua afya zao.
Mhe.Ester Mahawe mbunge viti maalumu CCM mkoa wa Manyara, akikabidhi shuka Waziri Jenista Mhagama alipofika kuweka jiwe la msingi kituo cha Afya Mirerani Simanjiro Manyara.
Ester Mahawe mbunge viti maalumu CCM mkoa wa Manyara, alimwomba Waziri
Mhagama kujengwa kituo cha Afya ndani ya machimbo ili kunusuri watu wanaofanya kazi za uchimbaji pamoja na maji kupunguza adha kwa akinamama ya kutembea umbali mrefu km 30 baada ya kujengwa ukuta ndani.
Kwa upande wake Martha Umbulla mbunge viti maalumu CCM naye alisema uwepo kwa kituo hicho cha afya ni ni jambo moja akisisitiza kuwa kati ya vitu 170 hapa nchini vinavyofanya kazi vizuri ni 56 na kuomba kupatiwa wataalamu katika kituo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAID, Dr. Leonard Maboko
Mhe. Ester Mahawe Mbunge Viti maalumu Kulia na Martha Umbulla Mbunge wakiteta
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula, ambaye pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara (kushoto)akifuatilia mkutano
Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama akisalimia baadhi ya wananchi waliofika kupata huduma ya Afya kituo cha Mirerani Simanjiro..
Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama akiaga wananchi wa mji mdogo wa Mirerani baada ya kuwekwa jiwe la msingi
Wananchi 49,802 kunufaika na kituo
cha afya Mirerani.
Na, MOHAMED
HAMAD
Kukamilika
kituo pekee cha afya kilichopo mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, kitanufaisha wakazi elfu 49, 802 wa eneo hilo na maeneo mengine.
Wananchi hao
walilazimika kutumia gharama kubwa ya kusaka huduma hiyo katika wilaya na mikoa
ya jirani, jambo lililosababisha adha madhara makubwa yakiwemo maafa.
Akizungumza na
wananchi wa mji wa Mirerani hivi karibuni, Waziri wanchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
(Sera, Bunge, Ajira na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama, alisema wananchi
wapata huduma ya afya kwa wakati.
“Kasi ya
maambukizi ya Ukimwi ni kubwa hapa Mirerani kutokana na mwingiliano wa watu, shughuli
za kiuchumi na hasa uchimbaji wa madini, Kituo hiki cha afya kitakuwa msaada
mkubwa kwa wananchi.
Kwa Mujibu
wa taarifa za mwaka 2016-2017, kiwango cha maamukizi ya Ukimwi kwa Mkoa wa Manyara ni 2.3%, na eneo la
Mirerani ni 6.4%.kiwango ambacho ni kikubwa”.
Kufuatia
hali hiyo, Waziri Mhagama akatoa wito kwa wanaume hapa nchini kutowatumia wake
zao kama njia ya kujua afya zao, akisisitiza kuwa kutakuwa na mpango kabambe wa
upimaji wa VVU Ukimwi kwa wanaume.
Mkurugenzi mtendaji
wa TACAID, Dr. Leonard Maboko akiwa Mirerani, alieleza sababu ya kujengwa Kituo
hicho kuwa ni uhitaji wa wananchi ambao walimwomba katika moja ya kikao
alipofika hapo na kuwataka waanze hatua za awali.
“Tulikuwa katika
kikao hapa Mirerani..ilitokea mazungumzo, wajumbe wakasema wanahitaji kituo cha
afya, nilichosema mkijenga nusu yake nasi tutamalizia, baada ya kuona jitihada
hizo, TACAID tuliungana nao kukamilisha kituo”alisema Dr. Maboko.
Mkuu wa
Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula, ambaye pia alimwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Manyara alisema Serikali itahakikisha kutoa ushirikiano na makini
katika kukamilisha kituo hicho ili malengo yake yatimie.
Ester Mahawe
mbunge viti maalumu CCM mkoa wa Manyara, alimwomba Waziri
Mhagama kujengwa
kituo cha Afya ndani ya machimbo ili kunusuri watu wanaofanya kazi za uchimbaji
pamoja na maji kupunguza adha kwa akinamama ya kutembea umbali mrefu km 30
baada ya kujengwa ukuta huo.
Kwa upande
wake Martha Umbulla mbunge viti maalumu CCM naye alisema uwepo kwa kituo hicho cha
afya ni ni jambo moja akisisitiza kuwa kati ya vitu 170 hapa nchini vinavyofanya
kazi vizuri ni 56 na kuomba kupatiwa wataalamu katika kituo hicho.
Mwiaho.
Maoni
Chapisha Maoni