Wauguzi Kiteto wadai sh 77 mil za sare Mei 23, 2018 Pata kiungo Facebook X Pinterest Barua pepe Programu Nyingine Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumain Magesa, (katikati) akiwa Zahanati ya Ilkiushibour Kata ya Makame.. Na, MOHAMED HAMAD JUMLA ya wauguzi 103, Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wanalazimika kukopa fedha mitaani ili kununua sare kufuatia kutopewa fedha na Serikali, (uniform allowance). Zaidi ya sh 77 mil zinadaiwa Serikali toka mwaka 2012, ambapo watumishi hao wamekuwa wakinunua sare zao wenyewe ili waweze kuendelea na kazi. Akisoma risala siku ya wauguzi duniani, Aisha Kassim, (muuguzi) mbele ya Mkurugenzi mtendani wa halmashauri ya Wilaya, Tamim Mahmoud Kambona, alisema kukosa (uniform allowance) kunaondoa molari ya kazi kwa watumishi hao. “Mhe mgeni rasmi moja ya changamoto tuliyonayo wauguzi ni kutopewa (uniform allowance) toka mwaka 2012 kisheria, rejea waraka wa utumishi wa umma kumb Na. CB/128/271/01/110 wa mwaka 2008 ambao unataka kila muunguzi alipwe sh 120,000 kila mwaka. Baadhi ya watumishi kutopandishwa vyeo kwa wakati, kutolipwa fedha kwaajili ya masaa ya ziada, pamoja na uelewa mdogo wa jamii wanaozunguka hospitali hivyo kuingilia majukumu ya wauguzi na kusababisha usumbufu kwa wauguzi. Akijibu risala hiyo, Tamimu Mahmoud Kambona mgeni rasmi na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, aliwahakikishia watumishi hao kuwa atatumia mapato ya ndani kuondoa tatizo la sare kwawatumishi hao. Kuhusu uchache wa watumishi Kambona alisema, ameshafanya mazungumzo na katibu Mkuu Utumishi hivi karibuni na kuahidiwa kupokea watumishi jambo ambalo alidai haliwezi kuchukua muda mrefu. Katika kuboresha huduma hospitalini hapo, Mkurugenzi Kambona alimvua madaraka Ramadhani Maingu aliyekuwa mganga mfawidhi wa hospitali na kuahidi kumteua mwingine, huku Mariamu Nkanyanga aliyekuwa mhasibu naye akiondolewa na kuahidiwa kuletwa mwingine. Kitendo cha kuvuliwa madaraka kwa watumishi hao, kiliibua vifijo na vigelegele kwa zaidi ya dakika mbili kama ishara ya kutoridhishwa na uwatendaji hao walipokuwa katika madaraka hayo Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina baadhi ya wauguzi walisema kuna upendeleo wa wazi uliokuwa unafanywa na viongozi hao hasa katika kulipana posho pamoja na semina na sasa wanaamini mabadiliko yatafanya wawe sawa. “Tulinyanyasika sana watumishi wa idara ya afyya acha Mungu afanye yake..hebu ngoje tuone kwa mabadiliko haya naamini waliobaki watajifunza kwani kuna watu wa semina, chanjo, pamoja na maslahi mingine..wengine mmmm”alisema mmoja wa wauguzi hao Mwisho. Maoni
Maoni
Chapisha Maoni