Mkuu Wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga, amefanya kikao cha kazi cha wafanya Biashara wa Wilaya ya mbulu.
Lengo la kikao hicho ni mashine ya EFDs na ulipaji wa kodi pamoja na utoaji wa risiti za EFDs kwa wafanya Biashara.
Akiongea katika kikao hicho amewataka wafanya Biashara wote kulipa kodi na kuwa na mashine ya EFDs pamoja na risiti ili kuboresha uchumi kwenda uchumi wa viwanda.
Mkuu huyo ametoa siku saba kwa wafanya Biashara wasiokuwa na mashine ya EFDs baada ya hapo watachukuliwa hatua za kisheria.
Mkuu huyo amempa siku mkurugenzi siku tano kutenga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara kwani wengine kufanya Biashara maeneo ya stend ambayo imepigwa marufuku.
Mkuu huyo akijibu hoja ya malalamiko kuhusu halmashauri dhidi ya utozaji Wa ushuru amesema halmashauri kuwa na mashine ya EFDs endapo kama wanawatoza wafanyabiashara.
Mkuu Wa wilaya amepiga marufuku unywaji Wa pombe wakati Wa kazi ambapo alisema ni kinyume cha sheria
Hata hivyo ameliagiza jeshi la polisi kukagua magari kama yanakidhi vigezo, kwani magari ya mbulu hayafai kwa usafiri.
kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa community cetre..
Maoni
Chapisha Maoni