SAME WAPATA TUZO YA MAKAMU WA RAIS

TUZO YA MAKAMU WA RAIS YAITAMBUA WILAYA YA SAME.

👉🏼Wilaya ya Same imetambuliwa kwa jitihada ya kutunza mazingira wakati wa kilele cha siku ya mazingira duniani, iliyofanyika kitaifa Mnazi mmoja Dar es salaam, Tar. 05/06/2018.

👉🏼Tuzo na zawadi hizo zilitolewa kwa washindi 3 wajumla kitaifa ambapo vikundi vinavyotunza mazingira vilizawadiwa.

Makundi matatu yaliyoongoza katika uhamasishaji wa nishati mbadala na taasisi mbili zilizotambuliwa katika jitihada ya utunzaji wa mazingira, ambapo Wilaya ya Same ilikuwa pekee iliyopata Tuzo.

👉🏼Akipokea Tuzo hiyo, DC wa Same aliishukuru Wizara hiyo kwa kutambua jitihada zao na kuwa Tuzo hiyo imewaongezea ari ya kuhakikisha mazingira ya Same yanabadilika.

👉🏼Aliwashukuru wote walioshiriki kupelekea juhudi hizo kutambuliwa (Halmashauri, NGOs, Taasisi za serikali na dini, Vyuo, viongozi na wananchi wote.

👉🏼" Na sasa tunakamilisha mpango mkakati wa mazingira ambao utatuwezesha kuwa na dira ya pamoja kama Wilaya kuelekea Same tunayoitaka" Alisema DC huyo.

Tuzo hii hutolewa kila baada ya miaka miwili na ofisi ya Makamu wa Rais.

DC " Same is not same"

Maoni